Shalom Wapendwa,
Maskini tunao siku zote, lakini Yesu …..
Napenda kushirikiana nanyi katika ujumbe huu niliou-copy na kuu-edit kutoka kwenye kitabu kiitwacho KUTAWALA FEDHA NA MATUMIZI.
Biblia inasema “maana sikuzote mnao maskini pamoja nanyi, na kila mpendapo mwaweza kuwatendea mema; lakini mimi hamnami sikuzote.” – MARK 14:7. Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake maneno hayo baada ya mwanamke mmoja kumimina marhamu kwenye kichwa chake na wao wakaanza kunung’unikia tendo hilo. Ni kweli masikini tunao siku zote; Hivyo wasiwe ndiyo sababu, kikwazo au kisingizio cha kushindwa kumtendea jambo jema Bwana Yesu. Masikini hao wapo kwenye matumizi yako ya fedha, kwenye muda wako na maamuzi mbali mbali.
Ninaposema maskini kwenye FEDHA zako ninamaanisha matumizi ya kila siku ya maisha; Kwenye MUDA wako ninamaanisha mambo ya kawaida ambayo unayafanya siku zote; Kwenye MAAMUZI yako ninamaanisha uchanguzi uliouzoelea siku zote; Hao ndiyo maskini ambao kila mtu anao na wapo siku zote. Je, maskini hawa wanakufanya ushindwe kufanya kitu cha tofauti katika maisha yako? Kunapotokea na maelekezo tofauti na ulivyozoea kufanya/kutumia fedha, umekuwa ukinung’unika (kama wanafunzi wa Yesu walivyomnung’unikia yule mwanamke)?
Nimesema kuwa matumizi kwa ajili ya maisha yapo siku zote hao ni MASKINI, ukiwaendekeza huwezi kufanya kitu cha tofauti katika maisha yako. Huwezi kuweka hata akiba, huwezi kuwekeza fedha nga kidogo ili ikuletee fedha zaidi. Wakati mwingine umekuwa ukisema na kuona kuwa maisha ni magumu sana na hivyo huwezi kufanya cho chote. Elewa kuwa ugumu wa maisha ni MASKINI wapo siku zote. Hivyo ugumu wa maisha usikufanye ushindwe kufanya kitu.
Yako mambo ambayo ni ya siku zote na ziko fursa ambazo hutokea kwa nadra sana. Mwanamke yule (Mariamu) aliiona fursa hiyo, akachukua marhamu akampaka Bwana kichwa chake. Bwana Yesu ali-conclude kwa kusema kuwa, “Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake. “ – MARK 14:9 (na leo nimelitaja). Lakini jambo la kujiuliza hapa ni kuwa huyu mwanamke alipata wapi fedha za kununulia marhamu ya bei kubwa namna hii. Jibu ni kuwa aliamua kuacha baadhi ya mambo na kuweka akiba hadi akafanikiwa kupata fedha hizo. Ukiwaendekeza hao maskini wako hutaweza kuweka kumbukumbu kwa ajili yako na uzao wako. Achia baadhi ya mambo, baadhi ya matumizi ya kila siku, baadhi ya maamuzi uliyoyazoea na chukua hatua mpya ya kubadilisha hali uliyonayo.
Hivyo katika fedha ulizo nazo na muda ulionao na uamuzi unaochukuwa unaweza kuubadilisha nga kidogo. Katika fedha hizo hizo unazopata ukaweka akiba nga kidogo; Katika muda huo huo unaobaki nao ukafanya jambo la tofauti nga kidogo; Na katika maamuzi hayo hayo, ukaamua maamuzi yanaweza kuufanya usijisikie comfortable nga kidogo. Kinachotakiwa ni kukubali kubadilika kwa kubadilisha mtazamo wako. Je utaendelea kuruhusu maskini ndio wawe sababu ya kukubakisha hapo ulipo? Uamuzi ni wako wa kuuza marhamu ili fedha zitakazopatikana uwape maskini au kuifungua marhamu hiyo na kuimimina juu ya kichwa cha Bwana Yesu!!!!
(Copied and Edited from the Book – Kutawala Fedha na Matumizi, Uk. 117-118; by Mathew D. Maduhu)
Filed under: MAFUNDISHO
