Quantcast
Channel: MAFUNDISHO – Strictly Gospel
Viewing all articles
Browse latest Browse all 46

Sio miaka yako bali siku zako!!

$
0
0

hesabu

Wapendwa SG,Nina neno nanyi ,nalo ni hili

SIO MIAKA YAKO BALI NI SIKU ZAKO

“Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima”. Zaburi 90:12

Kumbe kuna kupata hekima katika kuzihesabu siku zako. Unapenda kupata hekima hiyo hebu fuatana nami ktk maneno haya.

Wengi wetu kwenye group hii tumekwisha ishi siku elfu kumi na.. na tumebakiza siku elfu kumi na… Mungu anataka uhesabu siku zako, sio miaka yako!!

Kwanini? Kwa sababu ukihesabu miaka unaweza kuona miiingi kumbe ukiibadilisha kuwa siku …… ni kidogo tu. Hebu mchukulie mpendwa aliyeokoka/zaliwa miaka 40 iliyopita, anaweza kujiona kuwa ni wa zamaaani, kumbe hata siku elfu kumi na tano hana (ana siku 14,600 tuu). Kumbuka hata Mungu mwenyewe

anatambulishwa kama Mzee wa siku (Daniel 7:9,13&22).

Zaburi 90:10 inaonyesha wastani wa miaka ya mtu ni 80 sawa na siku elfu 29,200 (tufanye siku 30,000). Sasa hebu chukua miaka 80 toa miaka uliyoishi, umebaki na miaka mingapi? Je, 45, 50, 55 au 60? Mpendwa hiyo miaka iliyobaki unajua ni siku elfu kumi naa ..tu, ikizidi sana siku elfu ishirini?

Now, here comes the crucial question – Je, huoni kuwa hizo siku elfu kumi naa….zilizobaki ni chache? Shetani anafahamu muda aliyo nao ni mchache,

I guess huwa anahesabu siku! Wewe je, uko tayari kubadilisha mtazamo wako, hesabu siku zako how serious you are with the elfu kumi naaa days left? Jana imepita,

leo nayo hiyooo inapita ivi hivi tu?

How many days from your elfu kumi naa days left utakuwa –effective ktk utumishi wako. Biblia inaziita kabla hazijaja siku zilizo mbaya (Mhubiri 12:1).

Please take heed, kila siku ni ya maana sana, itumie vema usiiche iende zake hasa ukizingatia foleni za mjini zilivyo na ubize wake hapo napo ni mtihani wa visingizio.

Mpendwa Zipange, don’t lose easily any day, do something, say something worth it, significant  – NANUKUU “Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima; mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.” – EFESO 5:15-16.     GET IT?

Stay Protected,

Mathew.

 

 


Filed under: MAFUNDISHO

Viewing all articles
Browse latest Browse all 46

Trending Articles